Native Bible

1 Samuel 1:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa uchungu wa rohoni Hana alilia sana na akamwomba Bwana.

1 Samuel 1:10 in English

1 Samuel 1:10 · Berean Standard Bible

In her bitter distress, Hannah prayed to the LORD and wept with many tears.

Context

8Elikana mumewe akawa anamwambia, “Hana, kwa nini unalia? Kwa nini huli? Kwa nini kuvunjika moyo? Je, mimi si bora zaidi kwako kuliko watoto kumi?” 9Siku moja walipokuwa wamemaliza kula na kunywa huko Shilo, Hana alisimama. Wakati huo kuhani Eli alikuwa ameketi kwenye kiti pembeni mwa mwimo wa mlango wa Hekalu la Bwana. 10Kwa uchungu wa rohoni Hana alilia sana na akamwomba Bwana. 11Naye akaweka nadhiri, akisema, “Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, laiti ungeangalia huzuni kuu ya mtumishi wako na kunikumbuka mimi, wala usimsahau mtumishi wako nawe ukampa mwana, basi huyo mwana nitamtoa kwa Bwana kwa siku zote za maisha yake, wala wembe hautapita kichwani mwake.” 12Alipokuwa anaendelea kumwomba Bwana, Eli alichunguza kinywa chake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.