1 Wafalme 8:14
1 Kings 8:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kusanyiko lote la Israeli lilipokuwa limesimama hapo, mfalme akageuka na kuwabariki.
1 Kings 8:14 in English
1 Kings 8:14 · Berean Standard Bible
And as the whole assembly of Israel stood there, the king turned around and blessed them all
Context
12Ndipo Solomoni akasema, “Bwana alisema kwamba ataishi katika giza nene; 13naam, hakika nimekujengea Hekalu zuri sana, mahali pako pa kuishi milele.” 14Kusanyiko lote la Israeli lilipokuwa limesimama hapo, mfalme akageuka na kuwabariki. 15Kisha akasema:
“Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye kwa mkono wake mwenyewe ametimiza lile alilomwahidi Daudi baba yangu kwa kinywa chake mwenyewe. Kwa kuwa alisema, 16‘Tangu siku niliyowatoa watu wangu Israeli kutoka Misri, sikuchagua mji katika kabila lolote la Israeli ili Hekalu lijengwe humo ili Jina langu lipate kuwamo humo, bali nimemchagua Daudi kuwatawala watu wangu Israeli.’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.