Native Bible

1 Kings 8:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Makuhani walipoondoka katika Mahali Patakatifu, wingu likajaza Hekalu la Bwana.

1 Kings 8:10 in English

1 Kings 8:10 · Berean Standard Bible

And when the priests came out of the Holy Place, the cloud filled the house of the LORD

Context

8Mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba ncha zake zilionekana kutoka Mahali Patakatifu mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, lakini sio nje ya Mahali Patakatifu. Hiyo mipiko ipo hata leo. 9Ndani ya Sanduku hapakuwepo kitu kingine chochote isipokuwa zile mbao mbili za mawe ambazo Mose alikuwa ameziweka ndani yake huko Horebu, mahali ambapo Bwana alifanya Agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri. 10Makuhani walipoondoka katika Mahali Patakatifu, wingu likajaza Hekalu la Bwana. 11Nao makuhani hawakuweza kufanya huduma yao kwa sababu ya lile wingu, kwa kuwa utukufu wa Bwana ulijaza Hekalu lake. 12Ndipo Solomoni akasema, “Bwana alisema kwamba ataishi katika giza nene;

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.