1 Wafalme 7:47
1 Kings 7:47 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Solomoni akaviacha vitu hivi vyote bila kupima uzani wake, kwa sababu vilikuwa vingi sana hivi kwamba uzito wa shaba haungekadirika.
1 Kings 7:47 in English
1 Kings 7:47 · Berean Standard Bible
Solomon left all these articles unweighed, because there were so many. The weight of the bronze could not be determined.
Context
45masufuria, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia.
Vyombo hivi vyote ambavyo Huramu alimtengenezea Mfalme Solomoni kwa ajili ya Hekalu la Bwana vilikuwa vya shaba iliyongʼarishwa. 46Mfalme akaamuru wavisubu katika kalibu ya udongo wa mfinyanzi katika uwanda wa Yordani ulio kati ya Sukothi na Sarethani. 47Solomoni akaviacha vitu hivi vyote bila kupima uzani wake, kwa sababu vilikuwa vingi sana hivi kwamba uzito wa shaba haungekadirika. 48Solomoni pia akatengeneza samani zote zilizokuwa ndani ya Hekalu la Bwana:
madhabahu ya dhahabu;
meza ya dhahabu za kuweka mikate ya Wonyesho; 49vinara vya taa vya dhahabu safi (vitano upande wa kuume na vitano upande wa kushoto, mbele ya Patakatifu pa Patakatifu);
kazi ya maua ya dhahabu na taa na makoleo;
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.