1 Wafalme 5:4
1 Kings 5:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini sasa Bwana Mungu wangu amenipa utulivu kila upande hakuna adui wala maafa.
1 Kings 5:4 in English
1 Kings 5:4 · Berean Standard Bible
But now the LORD my God has given me rest on every side, and there is no adversary or crisis.
Context
2Solomoni akapeleka ujumbe huu kwa Hiramu: 3“Unajua kwamba kwa sababu ya vita vilivyopiganwa dhidi ya baba yangu Daudi kutoka pande zote, hakuweza kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana Mungu wake, hadi Bwana alipowaweka adui zake chini ya miguu yake. 4Lakini sasa Bwana Mungu wangu amenipa utulivu kila upande hakuna adui wala maafa. 5Kwa hiyo, ninakusudia kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana, Mungu wangu, kama Bwana alivyomwambia baba yangu Daudi, wakati aliposema, ‘Mwanao nitakayemweka kwenye kiti cha ufalme mahali pako, ndiye atajenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu.’ 6“Hivyo toa amri ili mierezi ya Lebanoni ikatwe kwa ajili yangu. Watu wangu watafanya kazi na watu wako, nami nitawalipa watu wako kwa ujira wowote utakaoupanga. Unajua kwamba hatuna mtu yeyote mwenye ustadi katika kukata miti kama Wasidoni.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.