1 Wafalme 5:16
1 Kings 5:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
pamoja na wasimamizi 3,300 ambao walisimamia kazi hiyo na kuwaongoza wafanyakazi.
1 Kings 5:16 in English
1 Kings 5:16 · Berean Standard Bible
not including his 3,300 * foremen who supervised the workers.
Context
14Akawapeleka Lebanoni kwa zamu za watu 10,000 kwa mwezi, hivyo walikaa Lebanoni kwa mwezi mmoja na miezi miwili nyumbani. Adoniramu ndiye alikuwa kiongozi wa shokoa. 15Solomoni alikuwa na wachukuzi wa mizigo 70,000 na wachonga mawe 80,000 huko vilimani, 16pamoja na wasimamizi 3,300 ambao walisimamia kazi hiyo na kuwaongoza wafanyakazi. 17Kwa amri ya mfalme walitoa kwenye machimbo ya mawe, mawe makubwa, yaliyo bora kwa kujengea msingi wa nyumba yaliyochongwa kwa ajili ya Hekalu. 18Mafundi wa Solomoni, wa Hiramu na watu wa Gebali* walikata na kuandaa mbao na mawe kwa ajili ya ujenzi wa Hekalu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.