1 Wafalme 5:13
1 Kings 5:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mfalme Solomoni akakusanya wafanyakazi 30,000 kutoka Israeli yote.
1 Kings 5:13 in English
1 Kings 5:13 · Berean Standard Bible
Then King Solomon conscripted a labor force of 30,000 men from all Israel.
Context
11naye Solomoni akampa Hiramu kori 20,000* za ngano kama chakula kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, pamoja na mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa bathi 20,000.* Solomoni aliendelea kumfanyia Hiramu hivyo mwaka baada ya mwaka. 12Bwana akampa Solomoni hekima, kama alivyomwahidi. Palikuwepo na uhusiano wa amani kati ya Hiramu na Solomoni, na wote wawili wakafanya mkataba. 13Mfalme Solomoni akakusanya wafanyakazi 30,000 kutoka Israeli yote. 14Akawapeleka Lebanoni kwa zamu za watu 10,000 kwa mwezi, hivyo walikaa Lebanoni kwa mwezi mmoja na miezi miwili nyumbani. Adoniramu ndiye alikuwa kiongozi wa shokoa. 15Solomoni alikuwa na wachukuzi wa mizigo 70,000 na wachonga mawe 80,000 huko vilimani,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.