1 Wafalme 5:11
1 Kings 5:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
naye Solomoni akampa Hiramu kori 20,000* za ngano kama chakula kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, pamoja na mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa bathi 20,000.* Solomoni aliendelea kumfanyia Hiramu hivyo mwaka baada ya mwaka.
1 Kings 5:11 in English
1 Kings 5:11 · Berean Standard Bible
and year after year Solomon would provide Hiram with 20,000 cors of wheat * as food for his household, as well as 20,000 baths of pure olive oil.*
Context
9Watu wangu watayakokota kutoka Lebanoni hadi kwenye bahari, nami nitayafunga mafungu mafungu yaelee juu ya maji hadi utakapoelekeza. Huko nitayatenganisha, nawe utaweza kuyachukua. Wewe utakidhi haja yangu kwa kunipatia chakula kwa ajili ya watu wa nyumbani mwangu.” 10Kwa njia hii Hiramu akampa Solomoni miti yote ya mierezi na magogo ya misunobari kama alivyohitaji, 11naye Solomoni akampa Hiramu kori 20,000* za ngano kama chakula kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, pamoja na mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa bathi 20,000.* Solomoni aliendelea kumfanyia Hiramu hivyo mwaka baada ya mwaka. 12Bwana akampa Solomoni hekima, kama alivyomwahidi. Palikuwepo na uhusiano wa amani kati ya Hiramu na Solomoni, na wote wawili wakafanya mkataba. 13Mfalme Solomoni akakusanya wafanyakazi 30,000 kutoka Israeli yote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.