1 Wafalme 2:43
1 Kings 2:43 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa nini basi hukutunza kiapo chako kwa Bwana na kutii amri niliyokupa?”
1 Kings 2:43 in English
1 Kings 2:43 · Berean Standard Bible
So why have you not kept your oath to the LORD and the command that I gave you?”
Context
41Solomoni alipoambiwa kuwa Shimei ametoka Yerusalemu na kwenda Gathi na amekwisha kurudi, 42mfalme akamwita Shimei na kumwambia, “Je, sikukuapiza kwa Bwana na kukuonya kuwa, ‘Siku utakayoondoka kwenda mahali pengine popote, uwe na hakika utakufa?’ Wakati ule uliniambia, ‘Ulilolisema ni jema. Nitatii!’ 43Kwa nini basi hukutunza kiapo chako kwa Bwana na kutii amri niliyokupa?” 44Pia mfalme akamwambia Shimei, “Unajua katika moyo wako makosa uliyomtendea baba yangu Daudi. Sasa Bwana atakulipiza kwa ajili ya mabaya yako uliyotenda. 45Lakini Mfalme Solomoni atabarikiwa, na kiti cha ufalme cha Daudi kitakuwa imara mbele za Bwana milele.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.