1 Wafalme 2:21
1 Kings 2:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akasema, “Mruhusu Abishagi, Mshunami, aolewe na ndugu yako Adoniya.”
1 Kings 2:21 in English
1 Kings 2:21 · Berean Standard Bible
So Bathsheba said, “Let Abishag the Shunammite be given to your brother Adonijah as his wife.”
Context
19Bathsheba alipokwenda kwa Mfalme Solomoni kuzungumza naye kwa ajili ya Adoniya, mfalme alisimama kumlaki mama yake, akamwinamia na kuketi kwenye kiti chake cha ufalme. Akaamuru kiti cha ufalme kuletwa kwa ajili ya mama yake mfalme, naye akaketi mkono wake wa kuume. 20Bathsheba akamwambia mfalme, “Ninalo ombi moja dogo la kukuomba; usinikatalie.”
Mfalme akajibu, “Omba, mama yangu; sitakukatalia.” 21Akasema, “Mruhusu Abishagi, Mshunami, aolewe na ndugu yako Adoniya.” 22Mfalme Solomoni akamjibu mama yake, “Kwa nini uombe Abishagi, Mshunami, kwa ajili ya Adoniya? Ungeweza pia kuomba ufalme kwa ajili yake, kwani yeye ni ndugu yangu mkubwa: naam, kwa ajili yake, na kwa kuhani Abiathari na Yoabu mwana wa Seruya!” 23Mfalme Solomoni akaapa kwa Bwana, akasema: “Mungu na aniulie mbali, tena bila huruma, ikiwa Adoniya hatalipa kwa uhai wake kwa ajili ya ombi hili!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.