1 Wafalme 17:8
1 Kings 17:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha neno la Bwana likamjia, kusema,
1 Kings 17:8 in English
1 Kings 17:8 · Berean Standard Bible
Then the word of the LORD came to Elijah:
Context
6Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi na mkate na nyama jioni, naye akanywa maji kutoka kile kijito. 7Baada ya muda, kile kijito kikakauka kwa sababu mvua haikuwa imenyesha katika nchi. 8Kisha neno la Bwana likamjia, kusema, 9“Ondoka, uende Sarepta ya Sidoni na ukae huko. Nimemwagiza mjane katika sehemu ile akupatie chakula.” 10Hivyo akaenda Sarepta. Alipofika kwenye lango la mji, mjane alikuwa huko akiokota kuni. Akamwita na kumwambia, “Naomba uniletee maji kidogo kwenye gudulia ili niweze kunywa.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.