Native Bible

1 Kings 17:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Ondoka, uende Sarepta ya Sidoni na ukae huko. Nimemwagiza mjane katika sehemu ile akupatie chakula.”

1 Kings 17:9 in English

1 Kings 17:9 · Berean Standard Bible

“Get up and go to Zarephath of Sidon, and stay there. Behold, I have commanded a widow there to provide for you.”

Context

7Baada ya muda, kile kijito kikakauka kwa sababu mvua haikuwa imenyesha katika nchi. 8Kisha neno la Bwana likamjia, kusema, 9“Ondoka, uende Sarepta ya Sidoni na ukae huko. Nimemwagiza mjane katika sehemu ile akupatie chakula.” 10Hivyo akaenda Sarepta. Alipofika kwenye lango la mji, mjane alikuwa huko akiokota kuni. Akamwita na kumwambia, “Naomba uniletee maji kidogo kwenye gudulia ili niweze kunywa.” 11Alipokuwa anakwenda kumletea, akamwita akasema, “Tafadhali niletee pia kipande cha mkate.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.