1 Wafalme 14:1
1 Kings 14:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati ule Abiya mwana wa Yeroboamu akaugua,
1 Kings 14:1 in English
1 Kings 14:1 · Berean Standard Bible
At that time Abijah son of Jeroboam became ill,
Context
1Wakati ule Abiya mwana wa Yeroboamu akaugua, 2naye Yeroboamu akamwambia mke wake, “Nenda ukajibadilishe, ili watu wasijue kwamba wewe ni mke wa Yeroboamu. Kisha uende Shilo. Nabii Ahiya yuko huko, yule aliyeniambia kuwa nitakuwa mfalme juu ya watu hawa. 3Chukua mikate kumi, maandazi kadhaa na gudulia la asali na umwendee. Atakuambia kitakachotokea kwa kijana.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.