1 Wafalme 10:26
1 Kings 10:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Solomoni akakusanya magari ya vita na farasi. Alikuwa na magari 1,400 na farasi 12,000, ambayo aliyaweka katika miji ya magari na mengine akawa nayo huko Yerusalemu.
1 Kings 10:26 in English
1 Kings 10:26 · Berean Standard Bible
Solomon accumulated * 1,400 chariots and 12,000 horses,* which he stationed in the chariot cities and also with him in Jerusalem.
Context
24Dunia yote ikatafuta kukutana na Solomoni ili kusikia hekima ambayo Mungu alikuwa ameiweka katika moyo wake. 25Mwaka baada ya mwaka, kila mmoja ambaye alikuja alileta zawadi: vyombo vya fedha na dhahabu, majoho, silaha na vikolezi, farasi na nyumbu. 26Solomoni akakusanya magari ya vita na farasi. Alikuwa na magari 1,400 na farasi 12,000, ambayo aliyaweka katika miji ya magari na mengine akawa nayo huko Yerusalemu. 27Mfalme akafanya fedha kuwa kitu cha kawaida kama mawe huko Yerusalemu, mierezi akaifanya kuwa mingi kama mikuyu vilimani. 28Farasi wa Solomoni waliletwa kutoka Misri na kutoka Kue.* Wafanyabiashara wa mfalme waliwanunua kutoka Kue.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.