1 Yohana 4:11
1 John 4:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Marafiki wapendwa, kama Mungu alivyotupenda sisi, imetupasa na sisi kupendana.
1 John 4:11 in English
1 John 4:11 · Berean Standard Bible
Beloved, if God so loved us, we also ought to love one another.
Context
9Hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha pendo lake kwetu: Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kupitia kwake. 10Hili ndilo pendo: si kwamba tulimpenda Mungu, bali yeye alitupenda, akamtuma Mwanawe, ili yeye awe dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu. 11Marafiki wapendwa, kama Mungu alivyotupenda sisi, imetupasa na sisi kupendana. 12Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote. Lakini tukipendana, Mungu anakaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu. 13Tunajua kwamba twakaa ndani yake na yeye ndani yetu, kwa sababu ametupa sisi sehemu ya Roho wake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.