Native Bible

1 John 4:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Tunajua kwamba twakaa ndani yake na yeye ndani yetu, kwa sababu ametupa sisi sehemu ya Roho wake.

1 John 4:13 in English

1 John 4:13 · Berean Standard Bible

By this we know that we remain in Him, and He in us: He has given us of His Spirit.

Context

11Marafiki wapendwa, kama Mungu alivyotupenda sisi, imetupasa na sisi kupendana. 12Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote. Lakini tukipendana, Mungu anakaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu. 13Tunajua kwamba twakaa ndani yake na yeye ndani yetu, kwa sababu ametupa sisi sehemu ya Roho wake. 14Nasi tumeona na kushuhudia kwamba Baba amemtuma Mwanawe ili awe Mwokozi wa ulimwengu. 15Kila akiriye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, basi Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.