1 Yohana 2:6
1 John 2:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yeyote anayesema anakaa ndani yake hana budi kuenenda kama Yesu alivyoenenda.
1 John 2:6 in English
1 John 2:6 · Berean Standard Bible
Whoever claims to abide in Him must walk as Jesus walked.
Context
4Mtu yeyote asemaye kuwa, “Ninamjua,” lakini hazishiki amri zake, ni mwongo, wala ndani ya mtu huyo hamna kweli. 5Lakini mtu yeyote anayelitii neno lake, upendo wa Mungu umekamilika ndani yake kweli kweli. Katika hili twajua kuwa tumo ndani yake. 6Yeyote anayesema anakaa ndani yake hana budi kuenenda kama Yesu alivyoenenda. 7Wapendwa, siwaandikii ninyi amri mpya bali ile ya zamani, ambayo mmekuwa nayo tangu mwanzo. Amri hii ya zamani ni lile neno mlilosikia. 8Lakini nawaandikia amri mpya, yaani, lile neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu, kwa sababu giza linapita na ile nuru ya kweli tayari inangʼaa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.