Native Bible

1 John 2:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Basi katika hili twajua ya kuwa tumemjua, tukizishika amri zake.

1 John 2:3 in English

1 John 2:3 · Berean Standard Bible

By this we can be sure that we have come to know Him: if we keep His commandments.

Context

1Watoto wangu wapendwa, nawaandikia haya ili msitende dhambi. Lakini kama mtu yeyote akitenda dhambi, tunaye Mwombezi kwa Baba: ndiye Yesu Kristo, Mwenye Haki. 2Yeye ndiye dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, wala si kwa ajili ya dhambi zetu tu, bali pia kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote. 3Basi katika hili twajua ya kuwa tumemjua, tukizishika amri zake. 4Mtu yeyote asemaye kuwa, “Ninamjua,” lakini hazishiki amri zake, ni mwongo, wala ndani ya mtu huyo hamna kweli. 5Lakini mtu yeyote anayelitii neno lake, upendo wa Mungu umekamilika ndani yake kweli kweli. Katika hili twajua kuwa tumo ndani yake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.