Native Bible

1 Corinthians 8:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hivyo basi, kuhusu kula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu: Tunajua kwamba “Sanamu si kitu chochote kabisa duniani,” na kwamba “Kuna Mungu mmoja tu.”

1 Corinthians 8:4 in English

1 Corinthians 8:4 · Berean Standard Bible

So about eating food sacrificed to idols: We know that an idol is nothing at all in the world, and that there is no God but one.

Context

2Mtu yeyote anayedhani kwamba anajua kitu, bado hajui kama impasavyo kujua. 3Lakini mtu ampendaye Mungu, hujulikana naye Mungu. 4Hivyo basi, kuhusu kula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu: Tunajua kwamba “Sanamu si kitu chochote kabisa duniani,” na kwamba “Kuna Mungu mmoja tu.” 5Kwa kuwa hata kama wapo hao wanaoitwa miungu, kama wakiwa mbinguni au duniani (kama ilivyo kweli wapo “miungu” wengi na “mabwana” wengi), 6kwetu sisi yuko Mungu mmoja, aliye Baba, ambaye vitu vyote vyatoka kwake na kwa ajili yake sisi twaishi; na kuna Bwana mmoja tu, Yesu Kristo, ambaye kwa yeye vitu vyote vimekuwepo na kwa yeye tunaishi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.