1 Wakorintho 7:26
1 Corinthians 7:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa sababu ya shida iliyoko kwa sasa, naona ni vyema mkibaki kama mlivyo.
1 Corinthians 7:26 in English
1 Corinthians 7:26 · Berean Standard Bible
Because of the present * crisis, I think it is good for a man to remain as he is.
Context
24Ndugu zangu, kama kila mtu alivyoitwa, akae katika wito wake alioitiwa na Mungu. 25Basi, kuhusu wale walio bikira, mimi sina amri kutoka kwa Bwana, lakini mimi natoa shauri kama mtu ambaye ni mwaminifu kwa rehema za Bwana. 26Kwa sababu ya shida iliyoko kwa sasa, naona ni vyema mkibaki kama mlivyo. 27Je, umeolewa? Basi usitake talaka. Je, hujaoa? Usitafute mke. 28Lakini kama ukioa, hujatenda dhambi; na kama bikira akiolewa, hajatenda dhambi. Lakini wale wanaooa watakabiliana na matatizo mengi katika maisha haya, nami nataka kuwazuilia hayo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.