1 Wakorintho 7:23
1 Corinthians 7:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mlinunuliwa kwa gharama; msiwe watumwa wa wanadamu.
1 Corinthians 7:23 in English
1 Corinthians 7:23 · Berean Standard Bible
You were bought at a price; do not become slaves of men.
Context
21Je, wewe ulipoitwa ulikuwa mtumwa? Jambo hilo lisikusumbue. Ingawaje unaweza kupata uhuru, tumia nafasi uliyo nayo sasa kuliko wakati mwingine wowote. 22Kwa maana yeyote aliyeitwa katika Bwana akiwa mtumwa yeye ni mtu huru kwa Bwana, kama vile yeyote aliyekuwa huru alipoitwa yeye ni mtumwa wa Kristo. 23Mlinunuliwa kwa gharama; msiwe watumwa wa wanadamu. 24Ndugu zangu, kama kila mtu alivyoitwa, akae katika wito wake alioitiwa na Mungu. 25Basi, kuhusu wale walio bikira, mimi sina amri kutoka kwa Bwana, lakini mimi natoa shauri kama mtu ambaye ni mwaminifu kwa rehema za Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.