Native Bible

1 Corinthians 7:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Je, wewe ulipoitwa ulikuwa mtumwa? Jambo hilo lisikusumbue. Ingawaje unaweza kupata uhuru, tumia nafasi uliyo nayo sasa kuliko wakati mwingine wowote.

1 Corinthians 7:21 in English

1 Corinthians 7:21 · Berean Standard Bible

Were you a slave when you were called? Do not let it concern you—but if you can gain your freedom, take the opportunity.

Context

19Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu. Lakini kuzitii amri za Mungu ndilo jambo muhimu. 20Basi kila mmoja wenu na abaki katika hali aliyoitwa nayo. 21Je, wewe ulipoitwa ulikuwa mtumwa? Jambo hilo lisikusumbue. Ingawaje unaweza kupata uhuru, tumia nafasi uliyo nayo sasa kuliko wakati mwingine wowote. 22Kwa maana yeyote aliyeitwa katika Bwana akiwa mtumwa yeye ni mtu huru kwa Bwana, kama vile yeyote aliyekuwa huru alipoitwa yeye ni mtumwa wa Kristo. 23Mlinunuliwa kwa gharama; msiwe watumwa wa wanadamu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.