1 Wakorintho 6:3
1 Corinthians 6:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hamjui kwamba tutawahukumu malaika? Je, si zaidi mambo ya maisha haya?
1 Corinthians 6:3 in English
1 Corinthians 6:3 · Berean Standard Bible
Do you not know that we will judge angels? How much more the things of this life!
Context
1Kama mtu yeyote wa kwenu ana ugomvi na mwenzake, anathubutuje kuupeleka kwa wasiomcha Mungu ili kuamuliwa badala ya kuupeleka kwa watakatifu? 2Je, hamjui kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Nanyi kama mtauhukumu ulimwengu, je, hamwezi kuamua mambo madogo madogo? 3Hamjui kwamba tutawahukumu malaika? Je, si zaidi mambo ya maisha haya? 4Kwa hiyo kama kuna ugomvi miongoni mwenu kuhusu mambo kama haya, chagueni kuwa waamuzi, watu ambao wanaonekana hata sio wa heshima katika kanisa. 5Nasema hivi ili mwone aibu. Je, inawezekana kuwa miongoni mwenu hakuna mtu mwenye hekima ya kutosha kuamua ugomvi kati ya waaminio?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.