Native Bible

1 Corinthians 15:35 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini mtu anaweza kuuliza, “Wafu wafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani?”

1 Corinthians 15:35 in English

1 Corinthians 15:35 · Berean Standard Bible

But someone will ask, “How are the dead raised? With what kind of body will they come?”

Context

33Msidanganyike: “Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema.” 34Zindukeni mwe na akili kama iwapasavyo, wala msitende dhambi tena; kwa maana watu wengine hawamjui Mungu. Nasema mambo haya ili mwone aibu. 35Lakini mtu anaweza kuuliza, “Wafu wafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani?” 36Ninyi wapumbavu kiasi gani? Mpandacho hakiwi hai kama hakikufa. 37Mpandapo, hampandi mwili ule utakao kuwa, bali mwapanda mbegu tu, pengine ya ngano au ya kitu kingine.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.