1 Wakorintho 14:4
1 Corinthians 14:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Anenaye kwa lugha hujijenga mwenyewe, bali atoaye unabii hulijenga kanisa.
1 Corinthians 14:4 in English
1 Corinthians 14:4 · Berean Standard Bible
The one who speaks in a tongue edifies himself, but the one who prophesies edifies the church.
Context
2Kwa maana mtu yeyote anayesema kwa lugha, hasemi na wanadamu bali anasema na Mungu. Kwa kuwa hakuna mtu yeyote anayemwelewa, kwani anasema mambo ya siri kwa roho. 3Lakini anayetoa unabii anasema na watu akiwajenga, kuwatia moyo na kuwafariji. 4Anenaye kwa lugha hujijenga mwenyewe, bali atoaye unabii hulijenga kanisa. 5Ningependa kila mmoja wenu anene kwa lugha lakini ningependa zaidi nyote mtoe unabii. Kwa kuwa yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko anenaye kwa lugha, isipokuwa atafsiri, ili kanisa lipate kujengwa. 6Sasa ndugu zangu, kama nikija kwenu nikasema kwa lugha mpya nitawafaidia nini kama sikuwaletea ufunuo au neno la maarifa au unabii au mafundisho?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.