1 Wakorintho 14:2
1 Corinthians 14:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana mtu yeyote anayesema kwa lugha, hasemi na wanadamu bali anasema na Mungu. Kwa kuwa hakuna mtu yeyote anayemwelewa, kwani anasema mambo ya siri kwa roho.
1 Corinthians 14:2 in English
1 Corinthians 14:2 · Berean Standard Bible
For he who speaks in a tongue does not speak to men, but to God. Indeed, no one understands him; he utters mysteries in the Spirit.
Context
1Fuateni upendo na kutaka sana karama za roho, hasa karama ya unabii. 2Kwa maana mtu yeyote anayesema kwa lugha, hasemi na wanadamu bali anasema na Mungu. Kwa kuwa hakuna mtu yeyote anayemwelewa, kwani anasema mambo ya siri kwa roho. 3Lakini anayetoa unabii anasema na watu akiwajenga, kuwatia moyo na kuwafariji. 4Anenaye kwa lugha hujijenga mwenyewe, bali atoaye unabii hulijenga kanisa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.