1 Wakorintho 12:8
1 Corinthians 12:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Maana mtu mmoja kwa Roho hupewa neno la hekima na mwingine neno la maarifa kwa Roho huyo huyo.
1 Corinthians 12:8 in English
1 Corinthians 12:8 · Berean Standard Bible
To one there is given through the Spirit the message of wisdom, to another the message of knowledge by the same Spirit,
Context
6Kisha kuna tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule atendaye kazi zote kwa watu wote. 7Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote. 8Maana mtu mmoja kwa Roho hupewa neno la hekima na mwingine neno la maarifa kwa Roho huyo huyo. 9Mtu mwingine imani kwa huyo Roho na mwingine karama za kuponya kwa huyo Roho mmoja. 10Kwa mwingine matendo ya miujiza, kwa mwingine unabii kwa mwingine kupambanua roho, kwa mwingine aina mbalimbali za lugha, na kwa mwingine bado, tafsiri za lugha.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.