1 Wakorintho 10:9
1 Corinthians 10:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wala tusimjaribu Kristo, kama baadhi yao walivyofanya, wakafa kwa kuumwa na nyoka.
1 Corinthians 10:9 in English
1 Corinthians 10:9 · Berean Standard Bible
We should not test Christ,* as some of them did, and were killed by snakes.
Context
7Msiwe waabudu sanamu, kama baadhi yao walivyokuwa, kama ilivyoandikwa, “Watu waliketi chini kula na kunywa, kisha wakainuka kucheza na kufanya sherehe za kipagani.” 8Wala tusifanye uzinzi kama baadhi yao walivyofanya, wakafa watu 23,000 kwa siku moja. 9Wala tusimjaribu Kristo, kama baadhi yao walivyofanya, wakafa kwa kuumwa na nyoka. 10Msinungʼunike kama baadhi yao walivyofanya, wakaangamizwa na mharabu. 11Mambo haya yote yaliwapata wao ili yawe mifano kwa wengine, nayo yaliandikwa ili yatuonye sisi ambao mwisho wa nyakati umetufikia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.