1 Wakorintho 10:8
1 Corinthians 10:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wala tusifanye uzinzi kama baadhi yao walivyofanya, wakafa watu 23,000 kwa siku moja.
1 Corinthians 10:8 in English
1 Corinthians 10:8 · Berean Standard Bible
We should not commit sexual immorality, as some of them did, and in one day twenty-three thousand of them died.
Context
6Basi mambo haya yalitokea kama mifano ili kutuzuia tusiweke mioyo yetu katika mambo maovu kama wao walivyofanya. 7Msiwe waabudu sanamu, kama baadhi yao walivyokuwa, kama ilivyoandikwa, “Watu waliketi chini kula na kunywa, kisha wakainuka kucheza na kufanya sherehe za kipagani.” 8Wala tusifanye uzinzi kama baadhi yao walivyofanya, wakafa watu 23,000 kwa siku moja. 9Wala tusimjaribu Kristo, kama baadhi yao walivyofanya, wakafa kwa kuumwa na nyoka. 10Msinungʼunike kama baadhi yao walivyofanya, wakaangamizwa na mharabu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.