1 Nyakati 9:21
1 Chronicles 9:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Zekaria mwana wa Meshelemia alikuwa bawabu katika ingilio la Hema la Kukutania.
1 Chronicles 9:21 in English
1 Chronicles 9:21 · Berean Standard Bible
Zechariah son of Meshelemiah was the gatekeeper at the entrance to the Tent of Meeting.
Context
19Shalumu mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, pamoja na mabawabu wenzake kutoka jamaa yake ya Kora waliwajibika kulinda malango ya Hema, kama vile baba zao walivyokuwa wamewajibika kulinda ingilio la Maskani ya Bwana. 20Hapo zamani Finehasi mwana wa Eleazari alikuwa kiongozi wa mabawabu, naye Bwana alikuwa pamoja naye: 21Zekaria mwana wa Meshelemia alikuwa bawabu katika ingilio la Hema la Kukutania. 22Jumla ya waliochaguliwa kuwa mabawabu katika sakafu za kupuria nafaka walikuwa watu 212. Waliandikishwa kwa koo zao kwenye vijiji vyao. Mabawabu hawa waliwekwa katika nafasi zao za kuaminiwa na Daudi pamoja na mwonaji Samweli. 23Wao na wazao wao walikuwa viongozi wa kulinda malango ya nyumba ya Bwana, nyumba iliyoitwa Hema.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.