1 Nyakati 7:15
1 Chronicles 7:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake aliitwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Selofehadi, ambaye alikuwa na wasichana tu.
1 Chronicles 7:15 in English
1 Chronicles 7:15 · Berean Standard Bible
Machir took a wife from among the Huppites and Shuppites. The name of his sister was Maacah. Another descendant was named Zelophehad, who had only daughters.
Context
13Wana wa Naftali walikuwa:
Yahzieli, Guni, Yeseri na Shalumu; hao walikuwa wazao wa Bilha. 14Wana wa Manase walikuwa:
Asirieli alikuwa mzao wake kutokana na suria wake wa Kiaramu. Huyu suria akamzaa Makiri baba wa Gileadi. 15Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake aliitwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Selofehadi, ambaye alikuwa na wasichana tu. 16Maaka mkewe Makiri akamzaa mwana aliyemwita Pereshi. Jina la nduguye lilikuwa Shereshi. Wana wa Pereshi walikuwa Ulamu na Rakemu. 17Mwana wa Ulamu alikuwa:
Bedani.
Hawa ndio waliokuwa wana wa Gileadi mwana wa Makiri, mwana wa Manase.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.