Native Bible

1 Chronicles 5:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yote haya yaliwekwa katika kumbukumbu za ukoo wao wakati wa utawala wa Yothamu, mfalme wa Yuda na Yeroboamu mfalme wa Israeli.

1 Chronicles 5:17 in English

1 Chronicles 5:17 · Berean Standard Bible

All of them were reckoned in the genealogies during the reigns of Jotham king of Judah and Jeroboam king of Israel.

Context

15Ahi mwana wa Abdieli, mwana wa Guni, alikuwa ndiye kiongozi wa jamaa yao. 16Wagadi waliishi Gileadi, huko Bashani pamoja na vijiji vilivyoizunguka, pia katika nchi yote ya malisho ya Sharoni kote walikoenea. 17Yote haya yaliwekwa katika kumbukumbu za ukoo wao wakati wa utawala wa Yothamu, mfalme wa Yuda na Yeroboamu mfalme wa Israeli. 18Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase walikuwa na watu mashujaa 44,760 waliokuwa wameandaliwa kwa ajili ya vita: watu wenye nguvu, hodari wa kutumia ngao na upanga, mashujaa wa kutumia upinde, waliokuwa tayari kwa ajili ya kazi hiyo. 19Walipigana vita dhidi ya Wahagari, Yeturi, Nafishi na Nodabu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.