1 Nyakati 29:24
1 Chronicles 29:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Maafisa wote na mashujaa, pamoja na wana wote wa Daudi, wakaahidi kumtii Mfalme Solomoni.
1 Chronicles 29:24 in English
1 Chronicles 29:24 · Berean Standard Bible
All the officials and mighty men, as well as all of King David’s sons, pledged their allegiance to King Solomon.
Context
22Wakala na kunywa kwa furaha kubwa mbele za Bwana siku ile.
Wakamtawaza Solomoni mwana wa Daudi mara ya pili kuwa mfalme, wakamtia mafuta kwa ajili ya Bwana ili awe mfalme na Sadoki kuwa kuhani. 23Solomoni akaketi kwenye kiti cha enzi cha Bwana kuwa mfalme mahali pa Daudi baba yake. Akafanikiwa sana na Israeli wote wakamtii. 24Maafisa wote na mashujaa, pamoja na wana wote wa Daudi, wakaahidi kumtii Mfalme Solomoni. 25Bwana akamtukuza sana Solomoni mbele ya Israeli wote na kumvika fahari ya kifalme ambayo hakuna mfalme yeyote wa Israeli kabla yake aliwahi kuwa nayo. 26Daudi mwana wa Yese alikuwa mfalme wa Israeli yote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.