Native Bible

1 Chronicles 29:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Daudi mwana wa Yese alikuwa mfalme wa Israeli yote.

1 Chronicles 29:26 in English

1 Chronicles 29:26 · Berean Standard Bible

David son of Jesse was king over all Israel.

Context

24Maafisa wote na mashujaa, pamoja na wana wote wa Daudi, wakaahidi kumtii Mfalme Solomoni. 25Bwana akamtukuza sana Solomoni mbele ya Israeli wote na kumvika fahari ya kifalme ambayo hakuna mfalme yeyote wa Israeli kabla yake aliwahi kuwa nayo. 26Daudi mwana wa Yese alikuwa mfalme wa Israeli yote. 27Alitawala Israeli kwa miaka arobaini: huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu. 28Daudi akafa akiwa mzee mwenye umri mwema, akiwa ameshiba siku, utajiri na heshima. Naye Solomoni mwanawe akawa mfalme baada yake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.