1 Nyakati 28:17
1 Chronicles 28:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya nyuma, mabakuli ya kunyunyizia na vikombe, masinia; uzito wa dhahabu kwa ajili ya kila bakuli la dhahabu; uzito wa fedha kwa ajili ya kila bakuli la fedha;
1 Chronicles 28:17 in English
1 Chronicles 28:17 · Berean Standard Bible
the weight of the pure gold for the forks, sprinkling bowls, and pitchers; the weight of each gold dish; the weight of each silver bowl;
Context
15Uzito wa dhahabu kwa ajili ya vinara vya dhahabu na taa zake, kukiwa na uzito kwa ajili ya kila kinara na taa zake, pamoja na uzito wa fedha kwa ajili ya kila kinara cha fedha na taa zake, kulingana na matumizi ya kila kinara; 16uzito wa dhahabu kwa ajili ya meza ya mikate iliyowekwa wakfu, uzito wa fedha kwa ajili ya meza ya fedha; 17uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya nyuma, mabakuli ya kunyunyizia na vikombe, masinia; uzito wa dhahabu kwa ajili ya kila bakuli la dhahabu; uzito wa fedha kwa ajili ya kila bakuli la fedha; 18na uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya madhabahu ya kufukizia uvumba. Pia alimpa kielelezo kwa ajili ya gari, yaani, wale makerubi wa dhahabu waliokunjua mbawa zao na kuweka kivuli juu ya Sanduku la Agano la Bwana. 19Daudi akasema, “Hii yote, ninayo kwa maandishi kutoka mkononi mwa Bwana ulio juu yangu, naye amenipa ufahamu kwa ajili ya habari zote za kielelezo hiki.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.