1 Nyakati 27:32
1 Chronicles 27:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yonathani mjomba wa Daudi alikuwa mshauri, mtu mwenye ufahamu mkubwa na mwandishi. Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa akiwahudumia wana wa mfalme.
1 Chronicles 27:32 in English
1 Chronicles 27:32 · Berean Standard Bible
David’s uncle Jonathan was a counselor; he was a man of insight and a scribe. Jehiel son of Hachmoni attended to the sons of the king.
Context
30Obili Mwishmaeli alikuwa msimamizi wa ngamia.
Yedeya Mmeronothi alikuwa msimamizi wa punda. 31Yazizi Mhagri alikuwa msimamizi wa makundi ya kondoo na mbuzi.
Hawa wote ndio waliokuwa maafisa wasimamizi wa mali alizokuwa nazo Mfalme Daudi. 32Yonathani mjomba wa Daudi alikuwa mshauri, mtu mwenye ufahamu mkubwa na mwandishi. Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa akiwahudumia wana wa mfalme. 33Ahithofeli alikuwa mshauri wa mfalme.
Hushai Mwariki alikuwa rafiki wa mfalme. 34Baada ya Ahithofeli, Yehoyada mwana wa Benaya aliingia mahali pake kama mshauri wa mfalme pamoja na Abiathari.
Yoabu alikuwa ndiye jemadari wa majeshi ya mfalme.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.