Native Bible

1 Chronicles 21:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Basi Daudi akamlipa Arauna shekeli za dhahabu 600* kwa ajili ya ule uwanja.

1 Chronicles 21:25 in English

1 Chronicles 21:25 · Berean Standard Bible

So David paid Ornan six hundred shekels of gold * for the site.

Context

23Arauna akamwambia Daudi, “Uchukue huo uwanja. Mfalme bwana wangu na afanye lolote analopenda. Tazama, nitatoa maksai kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, vifaa vya kupuria kuwa kuni, pamoja na ngano kwa ajili ya dhabihu ya nafaka. Natoa hivi vyote.” 24Lakini Mfalme Daudi akamjibu Arauna, “La hasha! Lakini ninasisitiza kwamba nitalipa bei yake kamili. Sitachukua kilicho chako kwa ajili ya Bwana au kutoa sadaka ya kuteketezwa ambayo hainigharimu chochote.” 25Basi Daudi akamlipa Arauna shekeli za dhahabu 600* kwa ajili ya ule uwanja. 26Kisha Daudi akamjengea Bwana madhabahu mahali hapo, na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Akamwita Bwana naye Bwana akajibu maombi yake kwa moto toka mbinguni juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. 27Kisha Bwana akanena na yule malaika, naye akarudisha upanga wake katika ala yake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.