1 Nyakati 21:27
1 Chronicles 21:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha Bwana akanena na yule malaika, naye akarudisha upanga wake katika ala yake.
1 Chronicles 21:27 in English
1 Chronicles 21:27 · Berean Standard Bible
Then the LORD spoke to the angel, who put his sword back into its sheath.
Context
25Basi Daudi akamlipa Arauna shekeli za dhahabu 600* kwa ajili ya ule uwanja. 26Kisha Daudi akamjengea Bwana madhabahu mahali hapo, na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Akamwita Bwana naye Bwana akajibu maombi yake kwa moto toka mbinguni juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. 27Kisha Bwana akanena na yule malaika, naye akarudisha upanga wake katika ala yake. 28Wakati huo, Daudi alipoona kwamba Bwana amemjibu kule kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Arauna Myebusi, akatoa dhabihu huko. 29Maskani ya Bwana ambayo Mose aliitengeneza kule jangwani, pamoja na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa wakati huo vilikuwa viko mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.