1 Nyakati 2:3
1 Chronicles 2:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wana wa Yuda walikuwa: Eri, Onani na Shela. Hawa watatu walizaliwa kwake na mkewe Mkanaani, binti wa Shua. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa Bwana, kwa hiyo Bwana alimuua.
1 Chronicles 2:3 in English
1 Chronicles 2:3 · Berean Standard Bible
The sons of Judah: Er, Onan, and Shelah. These three were born to him by Bath-shua the Canaanite. Er, Judah’s firstborn, was wicked in the sight of the LORD, who put him to death.
Context
1Hawa ndio waliokuwa wana wa Israeli:
Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Zabuloni, 2Dani, Yosefu, Benyamini, Naftali, Gadi na Asheri. 3Wana wa Yuda walikuwa:
Eri, Onani na Shela. Hawa watatu walizaliwa kwake na mkewe Mkanaani, binti wa Shua. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa Bwana, kwa hiyo Bwana alimuua. 4Tamari, mkwewe Yuda, alimzalia wana wawili: Peresi na Zera. Yuda alikuwa na jumla ya wana watano. 5Wana wa Peresi walikuwa:
Hesroni na Hamuli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.