1 Nyakati 19:8
1 Chronicles 19:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Daudi aliposikia jambo hili, akamtuma Yoabu na jeshi lote la wapiganaji.
1 Chronicles 19:8 in English
1 Chronicles 19:8 · Berean Standard Bible
On hearing this, David sent Joab and the entire army of mighty men.
Context
6Waamoni walipotambua kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Hanuni na Waamoni wakatuma talanta 1,000* za fedha ili kukodisha magari ya vita pamoja na waendeshaji wa hayo magari ya kukokotwa na farasi, kutoka Aramu-Naharaimu,* Aramu-Maaka na Soba. 7Wakakodisha magari ya vita 32,000 yakiwa na waendeshaji wake, pamoja na mfalme wa Maaka na vikosi vyake, wakaja na kupiga kambi karibu na Medeba. Waamoni nao wakakusanyika toka miji yao, wakatoka ili kupigana vita. 8Daudi aliposikia jambo hili, akamtuma Yoabu na jeshi lote la wapiganaji. 9Waamoni wakatoka wakajipanga wakiwa tayari kwa vita langoni la mji wao, wakati wale wafalme wengine waliokuja nao walijipanga kwa vita uwanjani. 10Yoabu akaona kuwa mbele yake na nyuma yake kumepangwa vita; kwa hiyo akachagua baadhi ya vikosi vilivyo bora sana katika Israeli akavipanga dhidi ya Waaramu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.