Native Bible

1 Chronicles 19:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Waamoni walipotambua kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Hanuni na Waamoni wakatuma talanta 1,000* za fedha ili kukodisha magari ya vita pamoja na waendeshaji wa hayo magari ya kukokotwa na farasi, kutoka Aramu-Naharaimu,* Aramu-Maaka na Soba.

1 Chronicles 19:6 in English

1 Chronicles 19:6 · Berean Standard Bible

When the Ammonites realized that they had become a stench to David, Hanun and the Ammonites sent a thousand talents of silver * to hire for themselves chariots and horsemen from Aram-naharaim,* Aram-maacah, and Zobah.

Context

4Kwa hiyo Hanuni akawakamata watu wa Daudi, akawanyoa ndevu akakata nguo zao katikati kwenye matako, akawaacha waende zao. 5Mtu mmoja alipofika na kumpasha Daudi habari za watu hawa, akawatuma wajumbe wengine kuwalaki, kwa maana walikuwa wamevunjiwa heshima sana. Mfalme akasema, “Kaeni huko Yeriko mpaka ndevu zenu ziote, ndipo mje.” 6Waamoni walipotambua kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Hanuni na Waamoni wakatuma talanta 1,000* za fedha ili kukodisha magari ya vita pamoja na waendeshaji wa hayo magari ya kukokotwa na farasi, kutoka Aramu-Naharaimu,* Aramu-Maaka na Soba. 7Wakakodisha magari ya vita 32,000 yakiwa na waendeshaji wake, pamoja na mfalme wa Maaka na vikosi vyake, wakaja na kupiga kambi karibu na Medeba. Waamoni nao wakakusanyika toka miji yao, wakatoka ili kupigana vita. 8Daudi aliposikia jambo hili, akamtuma Yoabu na jeshi lote la wapiganaji.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.