Native Bible

1 Chronicles 12:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Watu wa nusu ya kabila la Manase, waliotajwa kwa majina ili waje kumweka Daudi kuwa mfalme, watu 18,000.

1 Chronicles 12:31 in English

1 Chronicles 12:31 · Berean Standard Bible

From the half-tribe of Manasseh:* 18,000 designated by name to come and make David king.

Context

29Watu wa Benyamini, ndugu zake Sauli, walikuwa 3,000; wengi wao walikuwa wameendelea kuwa waaminifu kwa Sauli mpaka wakati huo. 30Watu wa Efraimu, mashujaa hodari 20,800, watu waliokuwa maarufu katika koo zao. 31Watu wa nusu ya kabila la Manase, waliotajwa kwa majina ili waje kumweka Daudi kuwa mfalme, watu 18,000. 32Watu wa Isakari, waliofahamu majira na kujua kile ambacho Israeli inapasa kufanya, walikuwa viongozi 200, pamoja na jamaa zao wote chini ya uongozi wao. 33Watu wa Zabuloni, askari wenye uzoefu mkubwa walioandaliwa tayari kwa vita wakiwa na silaha za kila aina, ili kumsaidia Daudi kwa uaminifu thabiti, walikuwa 50,000.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.