Native Bible

1 Chronicles 12:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Watu wa Efraimu, mashujaa hodari 20,800, watu waliokuwa maarufu katika koo zao.

1 Chronicles 12:30 in English

1 Chronicles 12:30 · Berean Standard Bible

From Ephraim: 20,800 mighty men of valor, famous among their own clans.

Context

28na Sadoki, kijana shujaa na hodari, aliyekuwa pamoja na maafisa ishirini na wawili kutoka jamaa yake. 29Watu wa Benyamini, ndugu zake Sauli, walikuwa 3,000; wengi wao walikuwa wameendelea kuwa waaminifu kwa Sauli mpaka wakati huo. 30Watu wa Efraimu, mashujaa hodari 20,800, watu waliokuwa maarufu katika koo zao. 31Watu wa nusu ya kabila la Manase, waliotajwa kwa majina ili waje kumweka Daudi kuwa mfalme, watu 18,000. 32Watu wa Isakari, waliofahamu majira na kujua kile ambacho Israeli inapasa kufanya, walikuwa viongozi 200, pamoja na jamaa zao wote chini ya uongozi wao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.