Zekaria 9:10
Zechariah 9:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu na farasi wa vita kutoka Yerusalemu, nao upinde wa vita utavunjwa. Atatangaza amani kwa mataifa. Utawala wake utaenea kutoka bahari hadi bahari, na kutoka Mto Frati hadi mwisho wa dunia.
Zechariah 9:10 in English
Zechariah 9:10 · Berean Standard Bible
And I will cut off the chariot from Ephraim * and the horse from Jerusalem, and the bow of war will be broken. Then He will proclaim peace to the nations. His dominion will extend from sea to sea, and from the Euphrates * to the ends of the earth.
Context
8Lakini nitailinda nyumba yangu
dhidi ya majeshi ya wanyangʼanyi.
Kamwe mdhalimu hatashambulia watu wangu tena,
kwa maana sasa ninawachunga. 9Shangilia sana, ee Binti Sayuni!
Piga kelele, Binti Yerusalemu!
Tazama, Mfalme wako anakuja kwako,
ni mwenye haki, naye ana wokovu,
ni mpole, naye amepanda punda,
mwana-punda, mtoto wa punda. 10Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu
na farasi wa vita kutoka Yerusalemu,
nao upinde wa vita utavunjwa.
Atatangaza amani kwa mataifa.
Utawala wake utaenea kutoka bahari hadi bahari,
na kutoka Mto Frati hadi mwisho wa dunia. 11Kwako wewe, kwa sababu ya damu ya Agano langu nawe,
nitawaacha huru wafungwa wako
watoke kwenye shimo lisilo na maji. 12Rudieni ngome yenu, enyi wafungwa wa tumaini;
hata sasa ninatangaza kwamba
nitawarejesheeni maradufu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.