Native Bible

Zechariah 4:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Pia kuna mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume wa bakuli na mwingine upande wa kushoto.”

Zechariah 4:3 in English

Zechariah 4:3 · Berean Standard Bible

There are also two olive trees beside it, one on the right side of the bowl and the other on its left.”

Context

1Kisha malaika aliyezungumza nami akarudi na kuniamsha, kama mtu aamshwavyo kutoka usingizi wake. 2Akaniuliza, “Unaona nini?” Nikajibu, “Ninaona kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake na taa zake saba juu yake, tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwenye taa zote zilizo juu yake. 3Pia kuna mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume wa bakuli na mwingine upande wa kushoto.” 4Nikamuuliza malaika aliyezungumza nami, “Hivi ni vitu gani, bwana wangu?” 5Akanijibu, “Hujui kuwa hivi ni vitu gani?” Nikajibu, “Hapana, bwana wangu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.