Zekaria 4:11
Zechariah 4:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha nikamuuliza yule malaika, “Hii mizeituni miwili iliyoko upande wa kuume na wa kushoto wa kinara cha taa ni nini?”
Zechariah 4:11 in English
Zechariah 4:11 · Berean Standard Bible
Then I asked the angel, “What are the two olive trees on the right and left of the lampstand?”
Context
9“Mikono ya Zerubabeli iliweka msingi wa Hekalu hili, mikono yake pia italimalizia. Kisha mtajua ya kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote amenituma mimi kwenu. 10“Ni nani anayeidharau siku ya mambo madogo? Watu watashangilia watakapoona timazi mkononi mwa Zerubabeli.
“(Hizi saba ni macho ya Bwana ambayo huzunguka duniani kote.)” 11Kisha nikamuuliza yule malaika, “Hii mizeituni miwili iliyoko upande wa kuume na wa kushoto wa kinara cha taa ni nini?” 12Tena nikamuuliza, “Haya matawi mawili ya mizeituni karibu na hiyo mirija miwili ya dhahabu inayomimina mafuta ya dhahabu ni nini?” 13Akajibu, “Hujui kuwa haya ni nini?”
Nikamjibu, “Hapana, bwana wangu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.