Zekaria 11:10
Zechariah 11:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha nikachukua fimbo yangu inayoitwa Fadhili nikaivunja, kutangua Agano nililofanya na mataifa yote.
Zechariah 11:10 in English
Zechariah 11:10 · Berean Standard Bible
Next I took my staff called Favor and cut it in two,* revoking the covenant I had made with all the nations.
Context
8Katika mwezi mmoja nikawaondoa wachungaji watatu.
Kundi la kondoo likanichukia, nami nikachoshwa nao, 9nikasema, “Sitakuwa mchungaji wenu. Waache wanaokufa wafe na wanaoangamia waangamie. Wale waliobakia kila mmoja na ale nyama ya mwenzake.” 10Kisha nikachukua fimbo yangu inayoitwa Fadhili nikaivunja, kutangua Agano nililofanya na mataifa yote. 11Likatanguka siku hiyo, kwa hiyo wale waliodhurika katika kundi, waliokuwa wakiniangalia wakajua kuwa hilo lilikuwa neno la Bwana. 12Nikawaambia, “Mkiona kuwa ni vyema, nipeni ujira wangu, la sivyo, basi msinipe.” Kwa hiyo wakanilipa vipande thelathini vya fedha.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.