Wimbo 5:14
Song of Songs 5:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mikono yake ni fimbo za dhahabu iliyopambwa kwa krisolitho. Mwili wake ni kama pembe ya ndovu iliyongʼarishwa iliyopambwa na yakuti samawi.
Song of Songs 5:14 in English
Song of Songs 5:14 · Berean Standard Bible
His arms are rods of gold set with beryl. His body is an ivory panel bedecked with sapphires.
Context
12Macho yake ni kama ya hua
kandokando ya vijito vya maji,
aliyeogeshwa kwenye maziwa,
yaliyopangwa kama vito vya thamani. 13Mashavu yake ni kama matuta ya vikolezo
yakitoa manukato.
Midomo yake ni kama yungiyungi
inayodondosha manemane. 14Mikono yake ni fimbo za dhahabu
iliyopambwa kwa krisolitho.
Mwili wake ni kama pembe ya ndovu iliyongʼarishwa
iliyopambwa na yakuti samawi. 15Miguu yake ni nguzo za marmar
zilizosimikwa katika vitako vya dhahabu safi.
Sura yake ni kama Lebanoni,
bora kama miti yake ya mierezi. 16Kinywa chake chenyewe ni utamu,
kwa ujumla yeye ni wa kupendeza.
Huyu ndiye mpenzi wangu, huyu ndiye rafiki yangu,
ee binti za Yerusalemu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.