Wimbo 4:1
Song of Songs 4:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu! Ee, jinsi ulivyo mzuri! Macho yako nyuma ya shela yako ni kama ya hua. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi zikishuka kutoka Mlima Gileadi.
Song of Songs 4:1 in English
Song of Songs 4:1 · Berean Standard Bible
How beautiful you are, my darling— how very beautiful! Your eyes are like doves behind your veil. Your hair is like a flock of goats streaming down Mount Gilead.
Context
1Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu!
Ee, jinsi ulivyo mzuri!
Macho yako nyuma ya shela yako
ni kama ya hua.
Nywele zako ni kama kundi la mbuzi
zikishuka kutoka Mlima Gileadi. 2Meno yako ni kama kundi la kondoo waliokatwa manyoya sasa hivi,
watokao kuogeshwa.
Kila mmoja ana pacha lake,
hakuna hata mmoja aliye peke yake. 3Midomo yako ni kama uzi mwekundu,
kinywa chako kinapendeza.
Mashavu yako nyuma ya shela yako
ni kama vipande viwili vya komamanga.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.