Ruthu 2:6
Ruth 2:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Msimamizi akamjibu, “Ni yule Mmoabu aliyerudi kutoka nchi ya Moabu pamoja na Naomi.
Ruth 2:6 in English
Ruth 2:6 · Berean Standard Bible
The foreman answered, “She is the Moabitess who returned with Naomi from the land of Moab.
Context
4Papo hapo Boazi akarudi kutoka Bethlehemu, akawasalimu wavunaji, akasema, “Bwana awe nanyi!”
Nao wakamjibu, “Bwana akubariki.” 5Boazi akamuuliza msimamizi wa wavunaji, “Je, yule mwanamwali ni wa nani?” 6Msimamizi akamjibu, “Ni yule Mmoabu aliyerudi kutoka nchi ya Moabu pamoja na Naomi. 7Yeye aliomba, ‘Tafadhali niruhusu niokote na kukusanya miongoni mwa miganda nyuma ya wavunaji.’ Naye ameshinda shambani tangu asubuhi pasipo kupumzika, isipokuwa kwa muda mfupi kivulini.” 8Kisha Boazi akamwambia Ruthu, “Binti yangu, nisikilize. Usiende kuokota mabaki ya mavuno katika shamba lingine, na usiondoke hapa. Kaa hapa na hawa watumishi wangu wa kike.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.